Kunguni ni mdudu wa ajabu sana.
Mdudu huyu hupenda kuishi maeneo waishipo binaadamu kwa kuwa chakula chake kikubwa ni damu y a binaadamu. Wadudu hawa hupenda kuishi vitandani na kujificha katika vipenyo vidogovidogo vya kitanda,au sehemu zinazofanana na hizo.

Mdudu huyu humuuma binaadamu na kujificha kewa harka sana.Wengi wanaoumwa na mdudu huyu hawatambui ila kwa alama za uvimbe na muwasho unaobaki baada ya kuumwa.
Kinachostaajabisha sana kwa mdudu huyu ni kwamba, KUNGUNI anaweza kukaa hadi miezi 18 bila kula na akiwa hai.katika hali hii kunguni huwa bapa zaidi na kubadilika rangi kutoka nyekundu/kahawia na kuwa Mweupe.Na punde tu baada ya kupata chakula(damu) Hubadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida.