Kadhia ya kucheleweshwa kwa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu,imekuwa kikwazo kikubwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Kumekuwa na Mtafaruku mkubwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutokana na kuchelewa kwa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo.
Wanafunzi wengi wamejikuta katika wakati mgumu kwa kushindwa kusajiliwa,Vyuoni kwa kuwa hawajalipa Ada na huku Bodi ya mikopo ikiwaacha Njia panda na wasijue nini hatma yao..
Kwa takwimu zilizopo ni takribani wanafunzi 88,000 walioomba mkopo wa elimu ya juu kupiti Bodi ya mikopo Kwa wanafun ze wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Lakini hadi sasa kuna matumaini ya wanfunzi 25,000 tu ambao watapatiwa mkopo kati ya hao 11,300 ikiwa tayari wameshapataiwa katika baadhi ya vyuo hapa nchini na 14,000 bado.
Bado kuna pigo kubwa kwa maelfu ya Wanafunzi ambao hawatopata mkopo na kushindwa kuendelea na elimu ya juu kwani wengi wao ni watoto wa masikini na hawawezi kumudu gharama za kujisomesha katika ngazi ya elimu ya juu.
Tunaiomba serikali ya awamu ya tano iliangalie hili na watafakari ni kwa namna gani wataweza kuwapatia nikopo Wanafunzi waliobaki na wqahitaji.